Masharti ya kukaa Hostel

MASHARTI YA KUKAA HOSTELI

 

  1. Wanafunzi wote wanatakiwa kujisajili katika kitabu maalum cha hosteli siku ya kureport hosteli.
  2. Usafi wa ndani ya chumba utafanywa na wanafunzi wanaoishi ndani ya chumba hicho.
  3. Usafi wa choo utafanywa na wanafunzi watakaotumia vyoo hivyo.
  4. Gharama za umeme katika chumba zitagharamiwa na wanafunzi watakaokuwa wanatumia chumba husika.
  5. Gharama ya maji na takataka zitahusisha wanafunzi wote wanaoishi katika hoteli ya wanawake na wanaume kwa ujumla wao.
  6. Ni marufuku kutumia jiko la aina yeyote ndani ya hosteli. Mwanafunzi atakayepatikana na vifaa vyovyote vile vya kupikia atafukunzwa kuishi ndani ya hosteli na vifaa hivyo kuchukuliwa. Faini itatozwa kwa atakayekutwa na vifaa hivyo.
  7. Ni marufuku kupiga kelele, kufungulia redio kwa sauti kubwa, kutumia lugha ya matusi/chafu,kupigana na vitendo vingine kama hivyo katika hosteli. Mwanafunzi atakayepatikana na makosa yaliyotajwa hapo atakuwa amepoteza sifa ya kuishi hosteli.
  8. Wageni wote HAWARUHUSIWI kuingia ndani ya hostel.yeyote atakayevunja sheria atakuwa amepoteza sifa za kuishi hosteli hivyo atafukuwa mara moja.
  9. Mwisho kuingia ndani ya hosteli ni saa 4 usiku na mlango wa geti kuu utafungwa saa hiyo.
  10. Ulinzi wa vifaa katika hosteli ni jukumu la wanafunzi wanaoishi hosteli.
  11. Muda wa kuondoka hosteli kuelekea chuo ni kuanzia saa 12 kamili asubuhi hadi saa 1 kamili asubuhi kwa kutumia basi la chuo.

KUMBUKA

  • Wizi, uasherati, ulevi, kuoigana, matusi, utumiaji wa madawa ya kulevya,uvutaji wa sigara na matendo machafu yatakufanya UFUKUZWE CHUO.
  • Hairuhusiwi mwanafunzi kuishi na mke/mume au motto ndani ya hosteliza chuo. Ukigundulika adhabu ni kufukuzwa kuishi katika hosteli.
  • Uongozi una hiari ya kufanya ukaguzi wakati wote katika vyumba vya hostel.

 

 

…………………………………

MKUU WA CHUO

...........................................................................
Nyaishozi College of Health and Allied Sciences;
2 Nyaishozi College Street;
14126 Mbweni, KINONDONI;
P.O. Box 68049;
Dar es Salaam, TANZANIA
Tel: +255-22-2928725
Mobile: +255-745-009792
Email: info@nyaishozicollege.ac.tz